Sanda ya Jambazi
Riwaya hii, SANDA YA JAMBAZI, inaendeleza pale ilipoishia ile riwaya iliyowasisimua wengi, UKIMWONA MMALIZE!
Inspekta Sindi na Koplo Fideli, ambae hivi karibuni amepandishwa cheo na kuwa Sajenti, ndio waliokuwa wakishughulikia upelelezi katika riwaya hiyo na kukutana nao tena katika riwaya hii.
Jambazi linalohusika ni lile lile Malik Mbowe.
Katika kulifukuza jambazi hilo, Inspekta Sindi na Koplo Fideli walikaribia kulinasa; lakini jitu kama Malik Mbowe halinasiki kirahisi. Sindi alimtaka Malik aweke bastola yake chini na anyooshe mikono juu. Kwamba jambazi hilo lilifikia mwisho wake.
Malik alimpuuza.
“Hunipati kirahisi, Sindi,” alimwambia, papo hapo akafyatua risasi mbili, akaunyakua mkoba wake. Alipoanza kutimua mbio, Inspekta Sindi aliinua bastola yake akafyatua risasi moja tu.
Wote wawili, Inspekta Sindi na Koplo Fideli, walimwona akiangukia bondeni huku mkono wake ukishikilia bega lililojeruhiwa vibaya. Alipiga kelele nyingi za maumivu.
Hawakumwona tena!
Ni baada ya askari hao wawili kufika nyumbani kwa Perino na kushuhudia yaliyotokea ndipo Sindi alipoamua yasambazwe matangazo nchini nzima na picha yake, kwamba yeyote atakayemwona jambazi huyo, popote pale, ammalize japokuwa alikuwa na uhakika kuwa Malik asingeweza kutoka mle bondeni hai.
Alikosea sana! Malik alikuwa na roho ngumu kama ya paka. Japo alijeruhiwa vibaya lakini alipona. Na balaa alilozusha huko alikokwenda halisemeki!
Sasa endelea…
TZS 7,000
Angalia Maelezo